Tuesday, 26 April 2016

Ufugaji bora wa kuku wa asili


 

 



YALIYOMO                                             

 

 

                                                  1.0 UTANGULIZI

Ufugaji wa kuku ni moja kati ya njia madhubuti katika kupunguza umasikini kwa jamii zetu za kitanzania. Kaya nyingi zimekuwa zikijihusisha na kilimo na ufugaji usio na tija kiasi kwamba malengo na mpango mkakati wa MKUKUTA,KILIMO KWANZA pamoja na MATOKEO MAKUBWA SASA hayajafikiwa ikilinganiswa na makusudio na makisio ya ukuaji wa uchumi, mwananchi wa hali ya chini.
Jina la nchi (Tanzania) Mwaka
2011
2012
2013
2014
Kipato/Siku
740.4
827.5
910.4
955.1

(http://data.worldbank.org/indicator/NY.GDP.PCAP.CD)
Kwa mtiririko wa vipato hivyo kwa siku tangu mwaka 2011 hadi 2016, mwananchi wa kawaida anauwiwa vigumu sana katika kutimiza mahitaji yake ya msingi ya siku, kutokuwa na uwezo wa kusomesha watoto na kutokupata huduma bora za kiafya. Kwa mtazamo huu, jamii zetu kushirikiana na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ni lazima kuangazia katika utoaji wa elimu ya ujasiliamali mdogo mdogo kwa jamii na kuwapa msaada wa kitaalamu ili kutimiza adhma ya kupunguza umasikini nchini.
Kuku wa asili ambao wamekuwa wakifugwa kwa mazoea katika maeneo mengi ya Tanzania ni suluhu tosha la umasikini ikiwa watafugwa kwa kuzingatia kanuni bora za ufugani pamoja na uwezeshaji wa ushauri wa kitaalamu. Pia kwa ufugaji bora wa kuku wetu wa asili, vijana watajipatia ajira, kupunguza uzururaji na kujipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao wenyewe.
Pia serikali itakuwa na uwezo wa kukusanya kodi kwa wingi kwa kupitia waajiriwa katika mashamba ya kuku,usafirishaji wa mazao ya kuku, dawa na leseni za biashara.
Ufugaji wa kuku wa asili unaweza kupunguza tatizo la upungufu wa vyakula vyenye viini lishe vya protini nchini hususani vitokanavyo na wanyama au ndege. Ongezeko la watu limekuwa kubwa hadi kufikia zaidi ya milioni 40. Ongezeko hilo halilingani na kasi ya uzalishaji wa chakula kulingana na sense ya wanyama ya mwaka 2010. Ulaji wa nyama kwa kila raia kwa mwaka umekuwa mdogo zaidi ukilinganisha na maadhimio ya FAO. Hii inadhihirisha kuwa uzalishaji wetu ni duni na matatizo yatokanayo na lishe duni (Utapiamlo,Kilibatumbo) hayawezi kutoweka kirahishi katika nchi yetu.
Kwa kuyatambua hayo katika sura ya utangulizi, andiko hili limeangazia kuboresha ufugaji wa kuku wa asili na wenye tija katika taswira ya tasnia ya ufugaji bora na maendeleo ya wananchi na mifugo.
Kulingana na kiasi cha mtaji na malengo ya kikundi tajwa, idadi ya kuku wanaotarajiwa kufugwa ni 100 (1:10).Kwa matokeo mazuri na mafanikio katika ujasilimali huu wa ufugaji wa kuku wa asili, yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia.

1.1 Sifa na mambo muhimu ya kuzingatia:

       I.            Mitetea na Jogoo wazuri kutoka katika koo zinazosifika kwa uzalishaji
    II.            Mabanda bora yaliyojengwa kwa malighafi zipatikanazo kiurahisi
 III.            Usimamizi na huduma njuri kwa kuku
 IV.            Chakura bora cha kuku na cha kutosha.
    V.            Uzuiaji mzuri wa magonjwa ya kuku.
   Ikiwa mahitaji ya hapo juu yatafuatwa kikamilifu,mafanikio hayanabudi kukufuata katika ujasiliamali wako.

 2.0 MAHITAJI MUHIMU KWA AJILI YA KUANZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI

2.1Jedwali kuonesha idadi ya kuku wa kuanza nao na gharama ya kununulia

NAMBA
HITAJI
GHARAMA/KUKU
JUMLA YA FEDHA
1
MITETEA 90
10,000/=
900,000 /=
2
MAJOGOO 10
15,000/=
150,000/=

 2.2 Banda la kuku

Ukubwa wa banda la kufugia kuku inategemeana sana na idadi ya kuku uliotaraji kuanza nao, uwezo wa kifedha na matarajio ya upanukaji wa mradi wako kwa baadaye. Kwa kuzingatia vigezo tajwa, idadi ya kuku kwa eneo na nafasi ya kulia chakula kwa kila kuku, linaweza kujulikana kimahesabu ili kujua banda lako liwe na ukubwa wa kiasi gani.

2.2.1Makisio:

       I.            Idadi ya kuku watagao =90
Wastani wa mayai yatagwayo /mzunguko/ kuku =8
    II.            Wastani wa asilimia ya utotoaji/mzunguko =80
 III.            Wastani wa vifaranga/kuku/mzunguko (80%*8)=6.4
 IV.            Jumla ya vifaranga/ kuku 90/mzunguko (90*6.4) = 576

  2.2.2 Idadi ya kuku kwa mita 1 ya eneo:

JINSIA NA HATUA ZA UKUAJI
                     (IDADI YA KUKU /M2)
JUMLA YA ENEO (M2)
KUKU WANAOTAGA
KUKU 4 /M2
90/4 =22.5
MAJOGOO
JOGOO 3 /M2
10/3 =3.3
VIFARANGA (SIKU 0-14)
VIFARANGA 15 /M2)
576/15 =38.4

Hivyo basi, jumla ya eneo linalohitajika kulingana na idadi ya kuku iliyooneshwa hapo juu ni 64.2M2.
NB: kiasi cha eneo tajwa hapo juu ni kulingana na idadi ya kuku tarajiwa katika mzunguko mmoja wa uzalishaji tu. Kwa kuzingatia makisio ya uzalishaji kwa mwaka, ni lazima kuongeza eneo mara tano zaidi ya eneo la mwazo. Na kwa kila mzunguko mmoja wa uzalishaji eneo halisi litakuwa zaidi ya 64.2M2 kwasababu utahitaji eneo kulishia, kunyweshea na kutuzia chakula cha kuku. Hivyo basi, eneo la kuanzia kufugia ni 120M2.

3.0 UTENGENEZAJI WA CHAKULA, MIKAKATI YA ULISHAJI NA GHARAMA ZA CHAKULA.

3.1 Chakula cha kuku wanaotaga (Wiki ya 22 hadi 72).

INGREDIENT
INCLUSION LEVEL IN KGS
AVAILABLE CP
CALCULATEDCP
COST/KG  FEED
COST/ KG
MAIZE BRAN
46
8.9
4.094
450
     20,700.00
MAIZE MEAL
10
10
1
700
        7,000.00
SUNF SEED CAKE
10
44
4.4
1000
     10,000.00
RICE POLISHING
18
8
1.44
200
        3,600.00
FISH MEAL
11
65
7.15
300
        3,300.00
DCP
1
0
0
1250
        1,250.00
BONE MEAL
1
0
0
400
             400.00
SALT
1
0
0
500
             500.00
LIMESTONE
2
0
0
500
        1,000.00
TOTAL (KGS)
100

18.084

     47,750.00




3.2 Chakula cha Vifaranga (Siku ya 1 - 28)

INGREDIENT
INCLUSION LEVEL IN KGS
AVAILABLE CP
CALCULATED CP
COST/KG FEED
COST/ KG
MAIZE BRAN
39.5
8.9
3.5155
450
     17,775.00
MAIZE MEAL
11.5
10
1.15
700
        8,050.00
SUNF SEED CAKE
12.5
44
5.5
1000
     12,500.00
RICE POLISHING
15
8
1.2
200
        3,000.00
FISH MEAL
16.5
65
10.725
300
        4,950.00
DCP
1
0
0
1250
        1,250.00
BONE MEAL
1
0
0
400
             400.00
SALT
1
0
0
500
             500.00
LIMESTONE
2
0
0
500
        1,000.00
TOTAL (KGS)
100

22.0905

     49,425.00

3.3 Chakula cha kuku wanaokuwa ( Wiki ya 5  - 16 )

INGREDIENT
INCLUSION LEVEL IN KGS
AVAILABLE CP
CALCULATED CP
COST/KG FEED
COST/ KG
MAIZE BRAN
43
8.9
3.827
450
     19,350.00
MAIZE MEAL
12
10
1.2
700
        8,400.00
SUNF SEED CAKE
11
44
4.84
1000
     11,000.00
RICE POLISHING
17
8
1.36
200
        3,400.00
FISH MEAL
12
65
7.8
300
        3,600.00
DCP
1
0
0
1250
        1,250.00
BONE MEAL
1
0
0
400
             400.00
SALT
1
0
0
500
             500.00
LIMESTONE
2
0
0
500
        1,000.00
TOTAL (KGS)
100

19.027

     48,900.00

3.4 Ulishaji wa kuku.

Tofauti na wanyama wengine, kuku wanahitaji kupewa chakula bora chenye mchanganyiko mzuri wa viinilishe kwasababu ya aina ya ukuaji wao ambao hutegemea sana chakula bora katika hatua ya ukifaranga, ukuaji, hatua ya mwisho ya ukuaji na kipindi cha utagaji. Chakula bora cha kuku husaidia ukuaji mzuri wa mifupa na misuli. Ulishaji mzuri wa kuku utamsaidia kuku katika maendeleo mazuri ya kinga za mwili, utagaji mzuri na ongezeko la utagaji wa mayai bora.
Kuku hulishwa mara moja kwa siku na kiasi cha chakula kwa kuku lazima kifuate umri wa kuku na mahitaji katika ukuaji, na uzalishaji.

3.5 Maji ya kunywa ya kuku.

Kama viinilishe vingine, maji ni hitaji la kwanza muhimu la kuku. Maji yana umuhimu mkubwa wa kibaiologia, kikemia, kimakenika na kazi zingine katika mwili wa kila kiumbe hai, katika hatua zote za uhai wake duniani. Hivyo basi, ni muhimu sana kwa kuku kupewa maji safi na yakutosha. Maji lazima yawepo muda wote. 
Water should be treated with chlorine before being admitted to chicken. It is important for the health status of the chicken because of E.coli found in the untreated water. 

3.6 Nafasi ya kulishia kwa (Tetea, kuku wanaotaga, Jogoo na Vifaranga)

Kabla ya kufanya maamuzi ya kununua vifaa vya kulishia kuku, ni muhimu kujua nafasi inayotumika kwa kuku mmoja kula. Ni muhimu pia kujua kuwa nafasi ya kulishia hutofautiana kati ya kifaranga, jogoo na tetea.

 3.6.1 Jedwali kuonyesha nafasi ya kulishia kuku katika hatua tofauti za ukuaji.

HATUA KATIKA UKUAJI
NAFASI YA KULISHIA KATIKA CM
Kifaranga
6
Tetea
9
Kuku wa kutaga
12
Jogoo
15

3.6.2 Gharama elekezi za vifaa vya kulishia na kunyweshea kuku.

KIFAA
UMBO
IDADI YA KUKU/KIFAA
GHARAMA / KIFAA
GHARAMA/ IDADI YA VIFAA TARAJIWA
Kifaa cha kulishia vifaranga
Dishi
50
10,000/=
576 chicks/50= 11*10,000=110,000/=
Kifaa cha kunyweshea vifaranga
Mviringo chenye mshikio
30
4,500/=
19*4500 =85,500/=
Kifaa kulishia kuku
 Mviringo chenye mshikio
10
5,500/=
10*5,500= 55,000/=
Poultry drinker




NB: Katika ufugaji wa kuku, chakula na ulishaji wa kuku huchukua 70% ya gharama zote za uzalishaji. Ni muhimu sana kufahamu hili kwasababu wafugaji wengi huwa na mafanikio duni katika ufugaji wa kuku kwasababu ya kutokutilia maanani kuhusu chakula cha kuku katika plani ya ufugaji na uwekezaji wao. Mfugaji yeyote atakaye thubutu kumudu gharama za chakula na chanjo hakika watafanikiwa katika uwekezaji wao.
Mfugaji lazima afahamu pia kwamba, matumizi mazuri ya chakula, maji na chanjo, hupunguza gharama za uzalishaji ambazo zitasaidia kuzalisha katika gharama ndogo na kupata faida nzuri.


4.0 USALAMA WA VIUMBE HAI NA UDHIBITI MATHUBUTI WA MAGONJWA.

Usalama wa viumbe hai ni mambo yote yafanyikayo katika shamba la kuku ili kuzuia wasishambuliwe na magonjwa au wadudu wasababishao magonjwa au vifo vya kuku shambani. Tunaweza kuzuia magonjwa au maambukizi kwa kufanya vitu vifuatavyo:
         I.            Ni muhimu chanjo zifanywe kwa muda na umri muafaka.
      II.            Tumia dawa za kuangamiza wadudu katika kuoshea vifaa au nyumba ya kuku kabla ya kuwaweka kwenye nyumba hiyo.
   III.            Watenge kuku walionunuliwa na kuwapa chanjo kabla hawajachanganywa na wenzao.
   IV.            Zuia watu wasiohusika na wanyama wengine wasiingie katika nyumba ya kuku.
      V.            Kuku wagonjwa wanapasa kutengwa mara moja na kutibiwa wakiwa peke yao.
   VI.            Kuku waliokufa ni lazima wafukiwe katika shimo la mizoga.
VII.            Kuku wa umri tofauti ni muhimu wakae tofauti.

       4.1 Mpangilio wa chanjo kwa kuku wazazi.

Katika ufugaji wa kuku, kinga ya magonjwa ni muhimu sana kuliko kutibu. Mkakati mzuri wa utunzaji wa kuku unahusisha sana chanjo na chakula. Ikiwa chanjo zitafanyika kiufasaha, afya za kuku zitaimarika kwa 95%  na 5% tu ndio itakayokuwa ni gharama ya matibabu.

4.1.1 Jedwali kuonesha mpangilio wa chanjo na gharama kwa kila chanjo.

No.
UMRI
CHANJO
SEHEMU
GHARAMA
1
Siku 1
mareks
Katikati ya ngozi na nyama

2
Siku 3
Newcastle
Tone kwenye jicho/ maji ya kunywa
6000/=/vial/vifaranga 100
3
Siku  7
paracox
Maji ya kunywa

4
Siku 12
IB-91
kunyunyiza

5
Siku 14
IBD-78
Maji ya kunywa

6
Siku 21
Newcastle
Eye drop/ drinking water
6000/=/vial/vifaranga 100
7
Siku 26
IBD-78
Maji ya kunywa

8
Siku 56
Salenvact
Katikati ya misuli ya kifua

9
Siku 70
AE +Fowl pox
Kwenye bawa

10
Siku 98
Salenvact
Katikati ya misuli ya kifua

11
Siku 120
IBH-120
Nyunyiza

12
Siku 126
MG (Microplasma gullisepticum)
Katikati ya ngozi na nyama


NB: Kila chanjo iliyo ainishwa hapo juu ni muhimu kwa afya za kuku. Hivyo basi, USIENDE ‘‘KINYUME NA MPANGILIO HUO

5.0 MAKISIO YA UZALISHAJI KWA MWAKA ANNUAL PRODUCTION ESTIMATE

MOTHS
No. F PS
No. EGGS/ HEN
TOTAL EGGS
% HATCH
No.CHICKS
No.CHICKS/HEN/CYCLE
MORTALITY %
LIVE CHICKEN
1
90
6
540
0.75
405
              4.5
0.14
348.3
2
90
7
630
0.75
472.5
5.25
0.14
406.35
3
90
8
720
0.8
576
6.4
0.14
495.36
4
90
8
720
0.82
590.4
6.56
0.14
507.74
5
90
8
720
0.82
590.4
6.56
0.14
507.74
6
90
8
720
0.82
590.4
6.56
0.14
507.74
7
90
8
720
0.82
590.4
6.56
0.14
507.74
8
90
8
720
0.82
590.4
6.56
0.14
507.74
SUBTOTAL


5490
0.8
4392
6.11875











9
180
8
1440
0.82
1180.8
13.12
0.14
1015.4
10
180
8
1440
0.82
1180.8
13.12
0.14
1015.4
11
180
8
1440
0.82
1180.8
13.12
0.14
1015.4
12
180
8
1440
0.82
1180.8
13.12
0.14
1015.4
 MAIN TOTAL

5760
0.82
4723.2
52.48
0.14
4061.9



Imeandaliwa na District Zoo Sanitary Inspector.
Mandela meckson Mwasikili
Musoma DC.


                                                                                                                               

1 comment:

Unknown said...

You are welcome for comments